Architecture March 05, 2026

Umuhimu wa picha za 3D kabla ya kuanza kumwaga zege site.

Site Visit

Teknolojia imebadilisha sekta ya ujenzi. Zamani, mteja alikuwa anaona ramani ya mistari tu (2D), lakini leo Blessedhand tunakupa uwezo wa "kutembea" ndani ya nyumba yako kabla hata msingi haujachimbwa.

Picha za 3D (3D Visualization) zinakusaidia kuelewa nafasi. Je, jiko linaingiliana vizuri na sehemu ya kulia chakula? Je, dirisha la chumba cha kulala linaangalia upande sahihi wa upepo na mwanga? Maswali haya yote yanajibiwa na 3D.

"Kurekebisha kosa kwenye kompyuta ni bure, lakini kurekebisha kosa kwenye jengo la zege ni mamilioni ya pesa."

Kuokoa Gharama za Ujenzi

Wateja wetu wengi wameepuka hasara ya kubomoa kuta baada ya kuona kuwa muonekano wa nje (Elevation) haukuwa vile walivyodhania. 3D inakupa uhakika wa 100% wa kile unachokilipia kwa mkandarasi wako.

Share this insight